Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anaelekea nchini Ujerumani, katika ziara inayolenga kuvutia wawekezaji na kuinadi biashara ya nchi yake.
Leo Modi atapokelewa kwa mazungumzo na Kansela Angela Merkel, katika mjini Berlin.
Mazungumzo yaliyokwama kuhusu mkataba wa biashara kati ya Umoja wa Ulaya na India maarufu kama BTIA, yanafikiriwa kuwa mojawapo ya agenda muhimu katika mkutano baina ya Merkel na Modi.
Ujerumani ndio mshirika muhimu zaidi wa India kibiashara kw asasa katika nchi za Ulaya.
Ubadilishanaji wa bidhaa na huduma baina ya nchi hizo ukifikia thamani ya euro bilioni 17.42 mwaka 2016.
