Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, ametembelea mji wa Mosul kuwapongeza wanajeshi katika kile alichokiita ukombozi wa mji huo kutoka kundi la wapiganaji wa kiislamu.
Hata hivyo, hakutangaza rasmi ushindi, akisema hilo litafanyika pindi vikundi vitakapobaki vitakapoondolewa.
Mosul ndipo kundi la wapiganaji wa kiislamu IS lilipotangaza kuunda uongozi wake miaka mitatu iliyopita.
Sehemu kubwa ya mji huo imekuwa vifusi baada ya mapigano ya miezi tisa ya kuwaondoa wapiganaji hao.
Bwana Abadi amekuwa akitembea katika barabara za mji wa Mosul na kuwapongeza wanajeshi.
