Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ameanza ziara rasmi katika mataifa ya Amerika Kusini.

In Kimataifa

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ameanza ziara rasmi katika mataifa ya Amerika Kusini.

 

Netanyahu aliondoka jana usiku katika uwanja wa ndege wa Tel Aviv kuelekea Argentina, kituo chake cha kwanza cha ziara hiyo.

 

Netanyahu ambaye ameandamana na mke wake Sara, ameieleza ziara yake kuwa ya kihistoria, kwa kuwa ni ya kwanza kuwahi kufanywa na waziri mkuu wa Israel huko Amerika Kusini.

 

Kutoka Argentina Netanyahu atazitembelea Colombia na Mexico, kabla kuelekea New York Marekani, ambako atauhutubia mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 26 mwezi huu.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Trump apiga marufuku raia wa mataifa 12 kuingia Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini tangazo jipya linaloweka marufuku kali kwa raia wa mataifa 12 kuingia nchini

Read More...

Serikali Yafuta Usajili wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Linaloongozwa na Askofu Gwajima

Serikali kupitia Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa, imetangaza kulifutia usajili Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na

Read More...

KATIBA YA CCM YAFANYIWA MABADILIKO 

Kwa mujibu wa taarifa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu