Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ameanza ziara rasmi katika mataifa ya Amerika Kusini.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ameanza ziara rasmi katika mataifa ya Amerika Kusini.

 

Netanyahu aliondoka jana usiku katika uwanja wa ndege wa Tel Aviv kuelekea Argentina, kituo chake cha kwanza cha ziara hiyo.

 

Netanyahu ambaye ameandamana na mke wake Sara, ameieleza ziara yake kuwa ya kihistoria, kwa kuwa ni ya kwanza kuwahi kufanywa na waziri mkuu wa Israel huko Amerika Kusini.

 

Kutoka Argentina Netanyahu atazitembelea Colombia na Mexico, kabla kuelekea New York Marekani, ambako atauhutubia mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 26 mwezi huu.

 

Exit mobile version