Waziri Mkuu wa Uingereza kupunguza vikwazo kwa mara ya kwanza nchini humo

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kwa mara ya kwanza ametangaza kupunguza vikwazo dhidi ya virusi vya corona. Johnson amesema kuanzia leo, watu ambao walikuwa hawawezi kufanya kazi wakiwa nyumbani, wanaweza kurudi kazini. Waziri Mkuu huyo pia amesema kuanzia Jumatano watu walio na jamaa zao majumbani wanaweza kutoka nje tena bora tu wadumishe kanuni za umbali wa mtu mmoja na mwengine. Amesema kuanzia Juni mosi, serikali yake itatoa tangazo la iwapo maduka yataanza kufunguliwa taratibu na iwapo wanafunzi wa shule za msingi wataweza kurudi shule. Johnson vile vile ametoa ruhusa ya watu kufanya mazoezi.

Exit mobile version