Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amewaacha mawaziri wake waandamizi katika nafasi zao wakati ameunda serikali mpya ya walio wachache akiungwa mkono na chama kidogo cha Ireland Kaskazini.
Chama cha May cha Conservative kilipoteza wingi wa viti bungeni katika uchaguzi wa kitaifa uliofanyika siku ya Alhamis ambao chama cha upinzani cha Labour kilinyakua zaidi ya viti vipya 30.
May sasa ataongoza serikali pamoja na chama cha siasa za mrengo wa kulia cha Democratic Unionist – DUP, ambacho viti vyake 10 vitampa wingi wa viti kwa ajili ya kuongoza.
Waziri huyo Mkuu aliitisha uchaguzi wa mapema katika jaribio la kuiimarisha nafasi yake katika Umoja wa Ulaya wakati Uingereza ikijiandaa kujiondoa katika Umoja huo.
Badala yake, Mbunge wa Labour David Lemmy anahisi kuwa uchaguzi huo umedhoofisha mamlaka yake.
