Waziri Ummy Mwalimu amteua Lwezimula kuwa Mkurugenzi wa MOI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, amemteua Dk.Respicious Lwezimula kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (MOI).

Nafasi hiyo ilikuwa inakaimiwa na Dk. Othman Kiloloma.

Dk Lwezimula anachukua nafasi hiyo iliyokuwa wazi tangu mwaka 2014, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MOI kustaafu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja, uteuzi huo umeanza jana.

Kabla ya uteuzi huo Dk Lwezimula alikuwa Daktari Bingwa katika Taasisi hiyo ya Mifupa ya MOI.

Exit mobile version