Waziri wa Elimu, Sayansi,Teknolojia na mafunzo ya ufundi Mh. Profesa Joyce Ndalichako amepiga marufuku shule ambazo hazijakamilika na kupewa kibali kupokea wanafunzi huku akitoa mwezi mmoja kwa shule ya sekondari Mwandiga wilayani Kigoma kukamilisha miundombinu ya shule hiyo ili ipokee wanafunzi wa kidato cha tano.
Mh Waziri Ndalichako ametoa kauli hiyo baada ya kukagua shule ya sekondari Mwandiga ambayo inatarajiwa kupokea kwa mara ya kwanza wanafunzi wa sayansi 143 wa kidato cha tano.
Hata hivyo profesa ndalichako ambapo ameagiza idara ya ukaguzi kufanya ukaguzi na kutoa kibali kabla shule kupokea wanafunzi hao.
Mapema Mkuu wa shule ya sekondari Mwandiga Albert Mutwe amesema kuwa shule hiyo inakabiliwa naukosefu wa huduma ya maji,bwalo, usafiri, nyumba za walimu na maktaba ya shule hiyo.
Naye mkuu wa wilaya ya Kigoma Samson Anga akiahidi kukamilisha miundombinu ya shule hiyo ili wanafunzi waweze kuanza kidato cha tano.
