Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed amesema sasa ni wakati muafaka kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuwekeza Visiwani Zanzibar ili kuchagiza juhudi za Serikali za kuwawezesha kiuchumi wakazi wa visiwa hivyo wanaojishughulisha na sekta za kilimo, uvuvi na uchakataji mazao.

Mhe. Hamad amesema Visiwa vya Zanzibar vina maeneo mengi ya uwekezaji yenye kuweza kuongeza tija na ongezeko la uchumi visiwani humo ikiwa kutakuwa na uwekezaji mkubwa katika maeneo hayo.

Kwa mujibu wa Mhe. Waziri, Zanzibar ni miongoni mwa visiwa vyenye utajiri mkubwa ambavyo kukiwa na uwekezaji wa kimkakati vinaweza kutokea matokeo makubwa na yenye kuwanufaisha wananchi wengi.

Akizungumza na Mhe. Waziri, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika  kilimo nchini.

Exit mobile version