Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ametoa tahadhari kubwa kwa watu ambao bado ,wanaendelea kujihusisha na vitendo vya ujangili ndani ya hifadhi za taifa zote nchini.
Ameyasema hayo wakati wa mahafali ya 52 na maadhimisho ya miaka 51 ya Taasisi ya Taaluma ya wanyamapori ya Pasiasi iliyoko mkoani Mwanza, nakusema kuwa wao kama Serikali wamejipanga kushinda Ujangili huo.
Aidha, ameongeza kuwa vijana wengi wanaomaliza katika vyuo hivyo wamefanikiwa kuwa kamata na kuwafikisha katika vyombo vya dola majangili wapatao 800, ambao wamekuwa wakijihusisha na shughuli hiyo.
Hata hivyo, kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho, Lowaeli Damalu amesema kuwa kutokana na mafunzo bora, Maaadili na Nidhamu wanayoitoa kwa wanafunzi wao,hivyo kuiomba Serikali kuwapatia Ajira Wahitimu katika Chuo hicho.
