WAZIRI wa Mambo ya dani ya Nchi MWIGULU NCHEMBA amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP)ERNEST MANGU kufuatilia tukio la askari polisi mmoja jijini Dar es Salaam aliyemtisha kwa risasi aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha ADAM MALIMA.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo MWIGULU amesema amelazimika kutoa agizo hilo ili ajue ukweli wa tukio hilo baada ya kupewa taarifa sahihi kwa sababu hadi sasa hajui suala hilo kwa undani.
Ameitaka jamii ivumilie kidogo wakati anasubiri taarifa hiyo na baadaye atatoa taarifa sahihi.

Wakati MWIGULU akisema hayo Mbunge wa Buyungu KASUKU BILAGO baada ya kipindi cha maswali na majibu ameomba muongozo kwa Mwenyekiti wa Bunge MUSSA ZUNGU akitaka kujua ni hatua gani zitachuliwa na Serikali ili kukabiliana na matumizi ya silaha hadharani.

akijibu muongozo huo ZUNGU amesema mpaka sasa  taarifa za tukio hilo hazijalifikia Bunge lakini kwa kuwa Serikali ipo bungeni na imelisikia, anaamini italifanyia kazi.

Exit mobile version