Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani ameituhumu Iran kufanya uchokozi wa hali ya juu.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson, ameituhumu Iran kwa kufanya uchokozi wa hali ya juu, ambao unanuia kuvuruga uthabiti katika Mashariki ya Kati na kuhujumu juhudi za Marekani katika kanda hiyo.
Rais Donald Trump tayari ameagiza tathmini mpya ifanywe, kuhusu mkataba uliotiwa saini kati ya nchi za Magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
Iran imekanusha mara kwa mara tuhuma kutoka kwa nchi za Magharibi kwamba inajaribu kustawisha silaha za nyuklia.

Exit mobile version