Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene amesema uchumi wa nchi ukitengemaa, serikali itaongeza posho za madiwani na watendaji wa vijiji.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene amesema uchumi wa nchi ukitengemaa, serikali itaongeza posho za madiwani na watendaji wa vijiji.

Simbachawene amesema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema).

Nassari alikuwa ametaka kusikia serikali itaongeza lini posho ya watendaji hao ambapo Simbachawene amesema, Serikali inatambua mchango wa viongozi hao katika maendeleo ya nchi, lakini kutokana na uchumi kutotengemaa, haiwezi kuwaongeza posho.

Akijibu swali la Mbunge wa Musoma Mjini, Vedasto Manyinyi (CCM), Naibu Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais (Tamesemi), Seleman Jafo alisema serikali inatambua mchango wao katika kusimamia shughuli za maendeleo. Katika swali lake la msingi, Manyinyi alitaka kujua kama serikali imeridhika na malipo ya wenyeviti wa mitaa na madiwani hao.

Jafo amesema majukumu yanayotekelezwa na viongozi hao ni utekelezaji wa dhana na ugatuaji wa madaraka, kwa wananchi ambapo mipango yote uamuzi unafanyika katika ngazi za msingi wa serikali za mtaa.

 

Exit mobile version