Waziri wa ulinzi wa Marekani aitaka Ufaransa kuendelea kupambana na ugaidi barani Africa.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Jim Mattis ameitaka Ufaransa kuendelea kupambana na ugaidi barani Afrika. Mattis ametoa wito huo baada ya ziara yake nchini Djibouti, eneo ambalo ni la mkakati wa jeshi la Marekani kwa bara la Afrika.

Aidha, amesema kuwa Marekani inaunga mkono Ufaransa katika vita dhidi ya magaidi katika eneo la Sahel hasa nchini Mauritania, Mali, Chad, Niger na Burkina Faso.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis allimuelezea rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh, wasiwasi wa Marekani kuhusu ujenzi wa kambi ya kwanza ya kijeshi ya China nje ya nchi, karibu na kambi ya Lemonnier ya jeshi la Marekani barani Afrika.

Marekani ina kambi moja peke barani Afrika ambayo imejengwa nchini Djibouti, na ina askari 4,000 kwa mujibu wa Pentagon.

 

Exit mobile version