Waziri wa ulinzi wa Marekani awasili Djibuti kwa ziara fupi.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Jim Mattis, amewasili Djibuti kwa ziara fupi, katika taifa la kimkakati la Pembe ya Afrika. Pia ni taifa pekee katika bara hilo lenye kambi ya kijeshi ya kudumu ya Marekani.

Kambi ya Lemonnier, iliyo na wanajeshi 4,000 wa Kimarekani na makandarasi ni muhimu kwa operesheni za kijeshi za Marekani inazozifanya nchini Somalia dhidi ya makundi ya wanamgambo kama vile al-Shabbab.

Kambi hiyo pia inasaidia operesheni za kijeshi za Marekani za nchini Yemen, ambapo vikosi maalumu vinafanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani ya mara kwa mara dhidi ya kundi la Al-Qaeda, katika Rasi ya Uarabuni.

Mattis anatarajiwa kukutana na rais wa Djibuti, Ismail Omar Gue lleh pamoja na Jenerali Thomas Waldha user, kamanda wa vikosi vya Marekani vilivyopo barani Afrika.

Exit mobile version