Waziri wa usalama nchini Kenya Jenerali Joseph Nkaissery amefariki dunia.

In Kimataifa
Waziri wa usalama nchini Kenya Jenerali Joseph Nkaissery amefariki dunia.
Habari kutoka Ikulu ya Nairobi imesema kuwa, Waziri Nkaissery alifariki dunia saa chache baada ya kulazwa ghafla katika hospitali ya Karen jijini Nairobi.
Kifo cha Nkaissery kimewashtua wakenya walio sikia  habari hii  kluhusiana na kifo cha waziri Nkaissery
Mara ya mwisho kuonekana hadharani ilikuwa siku ya Ijumaa wakati wa maombi ya wagombea urais katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi na kuonekana kuwa mwenye afya.
Kifo hiki kimetokea siku 30 kamili kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini humo.
Nkaissery aliteuliwa kuwa Waziri wa usalama mwaka 2014 akitokea chama cha upinzani cha ODM.
Kati ya mwaka 2008-2013 alikuwa Naibu Waziri wa Ulinzi katika serikali ya muungano.
Alikuwa mbunge wa zamani wa upinzani jimbo la Kajiado ya Kati kwa miaka 12.
Haijafahamika kilichosababisha kifo chake.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda

Read More...

WATOTO 109,514 KUPATIWA CHANJO YA MATONE DHIDI YA POLIO WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

Katika utekelezaji wa zoezi la Kampeni ya chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa  Polio, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi

Read More...

Tigo na mjasiriamali Boss yaja kukomboa wajasiriamali

Katika kuendelea kukuza utalii wa utamaduni hapa nchini kampuni ya Tigo kanda ya kaskazini imeendeleaa kuwaunga mkono wadau wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu