Baadhi ya madereva wa magari yanayofanya kazi katika mradi
wa ujenzi wa barabara inayoelekea katika mgodi wa makaa ya
mawe uliopo katika kata ya Luilo wilayani Ludewa mkoani
Njombe unaomilikiwa na kampuni ya Maxcol,wamedaiwa
kufanya wizi wa mafuta kwenye magari hayo wanayoendesha
kwa kushirikina na wananchi na kuyaingiza mtaani kwa ajili ya
biashara.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wananchi wa kata
hiyo mbele ya mkuu wa polisi wa wilaya ya Ludewa Deogratius
Massawe, wananchi hao wamekana kushirikiana na madereva
hao huku wakiwahusisha wageni ambao wameonekana kupanga
vyumba kwenye makazi yao wakidai kuwa ni wafanyakazi wa
mradi.
Hivyo wamewaomba polisi kuwapa ulinzi ili waharifu hao
wasije kuwadhuru kwa kutoa taarifa zao.