White House yasahihisha kauli ya Rais Trump kwamba angelipenda kukutana kwa Mzungumzo na Kim Jong.

 Ikulu ya Marekani, White House, imesahihisha kauli ya Rais Donald Trump kwamba, angelipenda kukutana kwa mazungumzo na mwenzake wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un.
Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Bloomberg hapo jana, Rais Trump amesema kwamba anaweza kukutana na hasimu wake huyo endapo mazingira yakiwa sawa.
Msemaji wa White House, Sean Spicer, amefafanuwa kwamba ili hilo litokezee, kuna masharti kadhaa ya kutimizwa, na ambayo hayana uwezekano wa kutekelezwa.
Hali ya wasiwasi kati ya nchi hizo mbili imeongezeka katika siku za hivi karibuni, huku kila upande ukionesha uwezo wake wa kijeshi.

 

Exit mobile version