Wito umetolewa kwa watendaji wa Mamlaka ya Maji safi Jijini Dar es
Salaam (DAWASCO) kuongeza nguvu katika usambazaji wa huduma hiyo kwani
katika hatua ya uzalishaji imeonesha mafanikio.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Profesa
Kitila Mkumbo wakati wa alipotembelea ofisi za Dawasco na kuzungumza
na watumishi wa Mamlaka hiyo, ambapo amewataka kuongeza kasi katika
usambazaji wa Maji na kuboresha miundombinu.
Aidha Profesa Mkumbo ametoa rai kwa Taasisi zisizolipia huduma hiyo
kusitishiwa mara moja kama ambavyo Agizo la Rais Magufuli kwa
wasiolipia huduma ya Umeme kusitishiwa.
Awali akiwasilisha ripoti ya hali ya utoaji huduma wa Mamlaka hiyo
Mkurugenzi Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa kwa sasa Mikoa ya
Dar es salaam na Pwani changamoto ya Huduma za maji safi zimepungua.
