Wito watolewa na Waziri wa Mambo ya nje wa China kuziondoa silaha za kinyuklia katika rasi ya korea.

Waziri wa mambo ya nje wa China ametoa wito wa kuondoa silaha za kinyuklia katika rasi ya Korea, huku mvutano juu ya mipango ya makombora na silaha za kinyuklia ya Korea Kaskazini ukiwa unazidi kupamba moto.

Wang Yi amewaambia maripota wa mjini Athens baada ya kukutana na mwenzake wa Ugiriki, Nikos Kotzias, kwamba China inaunga mkono kikamilifu kuondolewa kwa silaha zozote za kinyuklia katika eneo hilo, ili kupatikane utulivu na amani.

Rais wa Marekani Donald Trump ameitaka China kuchukua hatua imara, kuishinikiza Korea Kaskazini kusitisha mipango yake ya kinyuklia na makombora ya masafa marefu.

Katika wiki za hivi karibuni, Korea Kaskazini imekuwa ikitishia kujibu mashambulizi yoyote ya uchokozi.

Aidha shirika la habari la Yonhap la taifa hilo, limeripoti leo hii kwamba raia mmoja wa Kimarekani amekamatwa akiwa anajaribu kuikimbia Korea Kaskazini.

Ni raia wa tatu wa Kimarekani kushikiliwa nchini humo.

Exit mobile version