Wizara ya ulinzi nchini Kenya imeshutumu taarifa zilizokuwa zimeenezwa kwamba msemaji wa jeshi la Kenya Kanali Joseph Owuoth alikuwa ametoweka.

Wizara ya ulinzi nchini Kenya imeshutumu taarifa zilizokuwa zimeenezwa kwamba msemaji wa jeshi la Kenya Kanali Joseph Owuoth alikuwa ametoweka.

Waziri Raychelle Omamo, akihutubia wanahabari, amesema taarifa kama hizo zinatishia usalama na kuzua wasiwasi miongoni mwa maafisa wa jeshi na familia zao.

Kanali Owuoth aligonga vichwa vya habari baada ya kuthibitisha kwamba nyaraka zilizokuwa zimetumiwa na muungano wa upinzani nchini humo Nasa kudai kwamba serikali inapanga kutumia jeshi kutekeleza ‘mapinduzi’ ili kuendelea kusalia madarakani zilikuwa halisi.

Msemaji huyo hata hivyo alisema nyaraka hizo zilinukuliwa na kufasiriwa visivyo.

Bi Omamo, kwenye kikao hicho, alisema baada ya uchunguzi, imebainika kwamba nyaraka hizo zilizotumiwa na muungano wa Nasa zilikuwa ghush.

Exit mobile version