Maafisa katika mji wa Wuhan nchini China ambako janga la virusi vya corona lilianzia wamechukua hatua leo za kufanya uchunguzi kwa wakaazi wake milioni 11 wa mji huo kuhusu virusi vya corona katika muda wa siku 10 baada ya kugundulika kwa maambukizi kadhaa mapya.
Wakati huo huo mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza wa Marekani, Dr. Anthony Fauci ametoa tahadhari kwamba miji na majimbo inaweza kushuhudia vifo vingi zaidi vya ugonjwa wa COVID-19 pamoja na uharibifu wa uchumi iwapo yataondoa amri wa kubakia majumbani haraka, kinyume na rais Donald Trump anayetaka kufungua uchumi haraka.
Wasi wasi juu ya kuweka uwiano kati ya usalama wa watu dhidi ya virusi hivyo na kuporomoka kwa uchumi unaonekana katika mataifa mengi.
