Yanga kuzindua Uwanja wa Namfua kwa mabao tu!

Singida United imeipiga mkwara mzito Yanga, dhidi ya tambo zake za matumaini ya kuvuna pointi tatu katika Uwanja wa Namfua keshokutwa Jumamosi.

Singida inatarajia kuwakaribisha Yanga katika uwanja wake wa nyumbani katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu, huku Yanga wakitoa tambo za uhakika wa kuvuna pointi tatu dhidi ya Singida United ili kuwa vinara wa Ligi Kuu.

Singida united inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga Hans Pluijm, iko katika kiwango kizuri huku mwalimu huyo akichukulia mechi hiyo ya kawaida sana kutokana na kuwajua wachezaji wa klabu yake ya zamani.

Exit mobile version