Kikosi cha Yanga kimeendelea kujifua kwenye Uwanja wa Chai Chai mjini njombe, kabla ya kuikabili Majimaji mwishoni mwa wiki.
Jana Jumatatu jioni kocha wa Yanga George Lwandamina, aliwapa mazoezi mepesi nyota walioanza dhidi ya Njombe, huku wale waliokuwa benchi wakifanya mazoezi makali.
Kocha huyo raia wa Zambia amesema kuwa, kuna vitu vichache lazima wavifanyie kazi kabla ya kukabiliana na Majimaji ambayo ilitoka sare na Prisons wikiendi iliyopita.
Hata hivyo amesema hawezi kusema wazi ni marekebisho gani, lakini lazima waongeze nguvu kwenye vitu vya kiufundi.
