Zaidi ya Milioni 200 zimepatikana kutoka kwa wadau mbalimbali wanaoendelea kuchangia rambirambi kwa familia za wanafunzi 32, wa shule ya Lucky Vincent waliopoteza maisha kwenye ajali ya basi iliyotokea wiki iliyopita.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari ofisini kwake ,Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,amesema kuwa hadi sasa wamepokea kiasi cha Sh Milioni 215, kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Gambo amewataja wadau wengine kuwa ni Baraza la Wawakilishi
Zanzibar,Wizara ya Elimu Zanzibar,mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii pamoja na wadau wengine.
Amesema mpaka sasa zaidi ya Sh Milioni 190 zimetumika ikiwemo Sh Milioni 3,laki nane na elfu hamsini 850,000, kwa familia 32 zilizopoteza watoto wao katika ajali hiyo,gharama za mazishi ikiwemo magari na usafiri kwa ajili ya maziko yaliyofanyika katika mikoa ya Arusha,Iringa,Tanga,Mbeya na Kilimanjaro
