Zaidi ya wabunge 300 waitaka IMF,na benki ya dunia kufuta madeni ya nchi masikini.

In Kimataifa

Zaidi ya wabunge 300 kutoka duniani kote wamelitaka leo shirika la fedha ulimwenguni IMF na benki ya dunia kufuta madeni ya mataifa masikini kutokana na janga la virusi vya corona, na kuongeza hatua ya kuzipatia fedha ili kuepuka mdororo wa kiuchumi duniani.

Juhudi hizo, zikiongozwa na mgombea wa zamani wa kiti cha urais nchini Marekani seneta Bernie Sanders na mbunge wa baraza la wawakilishi Ilham Omar, wa chama cha Democratic kutoka jimbo la Minnesota, zinakuja wakati kuna wasi wasi mkubwa kwamba mataifa yanayoendelea pamoja na masoko yanayoinukia yataathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na janga la virusi vya corona.

Virusi hivyo vimewaambukiza watu zaidi ya milioni 4.2 duniani na kuwauwa watu 287,349, kwa ujibu wa idadi iliyokusanywa na shirika la habari la Reuters.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu