Mhalifu anaesafirisha wakimbizi kinyume na sheria amewatupa baharini zaidi ya wakimbizi 120 karibu na fukwe za mji wa Aden nchini Yemen.
Kwa mujibu wa manusura, kabla ya hapo jangili huyo aliwagundua watu waliovalia sare”. Shirika la kimataifa linalowahudumia wahamiaji IOM linasema wakimbizi 29 kutoka Somalia na Ethiopia wamezama.
Wengine 22 hawajulikani waliko, Mhalifu huyo akageuza njia baadae na kurejea Somalia ili kuwachukua wakimbizi wengine na kuwapeleka katika fukwe za Yemen-
Licha ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuenea maradhi yanayoambukiza ya kipindu pindu nchini Yemen; watu wasiopungua 55 elfu wamevuka ujia wa bahari mwaka huu kutoka pembe ya Afrika na kuingia Yemen, Baadhi yao wameelekea katika nchi tajiri za Ghuba kutafuta kazi.
