Zambia: Jeshi la polisi limemtia mbaroni kiongozi wa chama kidogo cha upinzani.

Jeshi la polisi nchini Zambia hapo jana limemtia mbaroni kiongozi wa chama kidogo cha upinzani nchini humo cha United Progressive Party ambaye ni mkosoaji wa Rais Edgar Lungu.

Kukamatwa kwa mwanasiasa huyo ni hatua ya hivi karibuni dhidi ya wapinzani wa kisiasa nchini Zambia.

Savior Chishimba ambaye ni kiongozi wa chama cha United Progressive Party alikamatwa na maafisa wa polisi baada ya kuonekana katika mahojiano kwenye kituo kimoja cha televisheni ya binafsi mjini Lusaka.

Rais wa Zambia Edgar Lungu mwezi uliopita alitangaza kuchukua hatua zaidi za kiusalama ambazo zinalipa mamlaka zaidi jeshi la polisi kuwatia mbaroni watu huku pia kiongozi huyo akivishutumu vyama vya upinzani nchini humo kwa kuhusika na vitendo vya vurugu.

Hakainde Hichilema kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zambia cha United Party for National Development amekuwa gerezani tangu mwezi April.

Rais Egar Lungu amekuwa akikanusha madai kuwa anajaribu kuunda utawala wa kiimla na anawashutumu mahasimu wake kisiasa kwa kutaka kubadilisha matokeo ya uchaguzi.

Exit mobile version