Ziara ya Rais wa Afrika Kusini nchini yazaa matunda.

In Kitaifa

Ziara ya Rais wa Afrika kusini  nchini imezaa matunda mara baada ya kusainiwa kwa mikataba mitatu ya ushirikiano katika sekta mbalimbali, zitakazosaidia kukuza uchumi wa nchi hizo mbili.

Mikataba hiyo imesainiwa Ikulu jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa marais Dkt. John Magufuli na Rais Jacob Zuma.

Nchi hizo mbili zimesaini hati ya muhtasari wa makubaliano ya mkutano wa tume ya pamoja ya Marais kati ya Tanzania na Afrika Kusini, uliolenga kuboresha makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mkutano huo.

Mikataba mingine ni hati ya makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya Bio Anuwai kati ya Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini, inayolenga kuboresha ushirikiano katika sekta ya wanyamapori na uhifadhi, na mkataba wa tatu ni hati ya makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya uchukuzi, kati ya Serikali ya Tanzania na Afrika kusini uliolenga kuboresha sekta ya uchukuzi.

Hata hivyo, katika mkutano huo Rais Magufuli amesema ziara ya Rais Zuma imekwenda sambamba na mkutano wa kwanza wa tume ya Marais, ambapo umebainisha baadhi ya maeneo ya makubaliano.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu