Kila nchi dunia huwa ina namba za dharura, ambazo hutumika kutolea taarifa yanapotokea matukio mbali mbali.
Hata hapa nchini kwetu zipo lakini sijui ni watu wangapi wanazifahamu na kuzitumia, pale tunapopatwa na majanga.
Sasa leo jeshi la zima moto na uokoaji nchini, limeendelea kuwasisitiza wananchi kuacha kutumia namba ya dharura ya 112 wanapokumbwa na majanga ya moto, na badala yake watumia namba ya 114.
Kwa kuitumia nmba hii ya 114, itakuwezesha kupata msaada wa moja kwa moja kutoka kwa jeshi hilo.
Hayo yamesemwa na mkuu wa jeshi hilo kamishana Thobias Adengenye, wakati akaizungumzia changamoto mbali mbali zinazolikabili jeshi hilo.
Baada ya kuzizungumzia changamoto hizo, ndipo akazungumzia uzinduzi wa namba mpya za dharura za jeshi hilo 114, ambazo wananchi wanapaswa kuzitumia pale majanga yanapojitokeza
