Serikali ya Zimbabwe imemuombea mkewe Mugabe kinga ya kidiplomasia,dhidi ya kesi ya ushambuliaji inayomkabili nchini Afrika kusini.
Mwanamitindo mwenye umri wa miaka ishirini nchini humo, amemtuhumu Bi Mugabe kwa kumshambulia, katika hoteli moja iliyopo mjini Johannesburg.
Polisi nchini humo wamesema kwamba,walitarajia Bi Mugabe angejiwasilisha kwao mwenyewe jana, lakini hakufanya hivyo.
Akizungumza mbele ya kamati ya bunge, kaimu mkuu wa polisi Leseja Mothiba, amesema Bi Mugabe ni lazima afikishwe mahakamani.
