Zitto: Nasubiri Polisi Wanipeleke Mahakamani.

Mbunge wa kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo Zito Kabwe, leo tena ameripoti katika Kituo cha Polisi Chang’ombe kuhusiana na tuhuma zinazomkali za kutumia lugha ya uchochezi.
Zitto anatuhumiwa kutumia luigha ya uchochezi wakati alipokuwa katika mkutano wake wa kampeni za udiwani huko Kijichi-Mbagala Dar.
Wakati akizungumza na wanahabari baada ya kutoka amesema kuwa amepewa maelekezo kwamba anatakiwa kuripoti Novemba 17 mwaka huu.
Pia amezungumzia juu ya katibu wake na Mwenyekiti wake wa chama, walioitwa katika kituo cha makosa ya uchunguzi wa fedha, kilichopo Kamata Kariakoo kuhusu takwimu walizozitoa za Pato la Taifa zinazodaiwa kuwa za uongo.

Exit mobile version