Zomeazomea yasababisha COSATU kukatisha hotuba ya Rais Zuma katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi nchini Afrika Kusini

 Muungano wa vyama vya wafanyakzi nchini Afrika Kusini Cosatu umelazimika kukatisha ghafla hotuba za kuadhimisha siku ya wafanyakazi ikiwemo hotuba iliyokuwa ikitarajiwa kutolewa na Rais Jacob Zuma baada ya umati kuanza vurugu na baadhi yao kumzomea Zuma.

Rais huyo na ujumbe wake walionekana wakiondoka haraka kutoka kwenye jukwaa la maadhimisho hayo na kuchukuliwa na msafara mkubwa wa magari.

Cosatu ambao ni mshirika muhimu kisiasa wa chama tawala cha Afrika Kusini African National Congress ANC mwezi uliopita ulimtaka Zuma kujiuzulu baada ya kumuachisha kazi waziri wa fedha na kusababisha kushushwa kwa uwezo nchi hiyo kukopesheka.

Misururu ya maandamano imefanyika nchini humo kwa miezi kadhaa sasa kumshinikiza Zuma kuachia madaraka kutokana na kashfa za ufisadi na uongozi mbovu.

 

Exit mobile version