Rais wa Afrika Kusini anayekumbwa na kashfa Jacob Zuma, ameondoka kwenye mkutano wa siku ya kimataifa ya wafanyazi baada ya kukemewa na wafanyakazi wanaomtaka ajiuzulu.
Fujo zilizuka kati ya wafuasi wa Bwana Zuma na wapinzani na kusabababisha hotuba yake kufutwa.
Chama kikuu cha wafanya kazi Cosatu, kilimtaka Bwana Zuma ajiuzulu mwezi uliopita baada ya kumfuta kazi waziri wa fedha aliyekuwa akiheshimiwa sana.
Bwana Zuma ameapa kusalia ofisini hadi muhula wake ukamilike mwaka 2019.
