Handeni kuwa ya mfano ufugaji wa kisasa-Ulega.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema
Serikali imeweka mipango mizuri ya kuhakikisha kijiji cha
Msomera kilichopo Wilayani Handeni, Mkoani Tanga kinakuwa
na miundombinu ya kisasa ya kuhudumia mifugo ikiwemo
Majosho, Malambo na Nyanda za malisho ili wafugaji kutoka
hifadhi ya Ngorongoro watakaohamia katika eneo hilo waweze
kufuga kisasa na kwa tija.


Ulega aliyasema hayo alipofanya ziara katika Kijiji hicho cha
Msomera ambapo kuna eneo limetengwa maalum kwa ajili ya

wafugaji kutoka hifadhi ya Ngorongoro kuhamia hapo kwa hiari
yao ili kuendeleza shughuli zao za ufugaji.

Exit mobile version