MADELEKA AIKIMBIA CHADEMA, AJIUNGA NA ACT

Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita, ametangaza rasmi kujiunga kwa Wakili Peter Madeleka na chama hicho akitokea Chadema. Madeleka amekabidhiwa kadi ya uanachama na katiba ya chama kama ishara ya kupokelewa rasmi.

Hafla hiyo imefanyika leo Mei 20, 2025 katika makao makuu ya chama hicho Magomeni, Dar es Salaam. Isihaka amempongeza Madeleka kuwa ni mpigania haki za wananchi.

Akizungumza baada ya kupokelewa, Wakili Madeleka amesema ameamua kujiunga na ACT Wazalendo ili kuimarisha nguvu ya upinzani na kuwapa Watanzania matumaini ya mabadiliko. Amesisitiza umuhimu wa kupigania demokrasia na haki za binadamu kwa njia mbalimbali.

Exit mobile version