Mapigano kati ya makundi pinzani ya Libya mashariki mwa Tripoli yameingia siku ya pili jana

Mapigano kati ya makundi pinzani ya Libya mashariki mwa Tripoli yameingia siku ya pili jana, na kuwazuia wakaazi kurejea majumbani kwao.
Mapigano yalizuka Jumapili wakati makundi yenye silaha yanayoipinga serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa mjini Tripoli yalijaribu kuingia katika mji huo mkuu na wakakabiliwa na makundi hasimu ambayo yanaegemea upande wa serikali hiyo.
Wizara ya afya ya Libya imethibitisha kuwa karibu watu wanne wameuawa na wengine 21 wamejeruhiwa katika mapigano hayo.
 Serikali ya Umoja wa Kitaifa imeshindwa kuweka utulivu tangu ilipowasili mjini Tripoli Machi mwaka jana. Serikali hiyo inapingwa na makundi ambayo yanadhibiti mashariki mwa Libya, ambako kamanda wa kijeshi Khalifa Haftar amekuwa akiimarisha nafasi yake kwa kuwateua mameya.
Exit mobile version