Ndege ya mizigo Boeing 767-300F kutua April.

Serikali inatarajia kupokea ndege ya kwanza ya Mizigo ili
kutatua changamoto za wafanyabiashara za usafirishaji wa
mizigo duniani.


Akizungumza Jijini Dar es Salaam kwenye ufunguzi wa
Mkutano wa mwaka 2022/23 wa wadau wa ATCL wa
Usafirishaji Mizigo Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu,
amesema ujio wa ndege hiyo nchini utawezesha waliokuwa
wanalazimika kupeleka mizigo yao nje ya nchi kupitia ndege za
nchi jirani,sasa hawata lazimika kufanya hivyo.

Exit mobile version