NMB yatoa gawio la shilingi bilioni 15 kwa Serikali.


Taarifa kutoka jijini Dodoma leo August 19 ni kwamba Waziri
wa Fedha na Mipango Dokta Philip Mpango amepokea gawio la
Serikali kutoka Benki ya NMB gawio la shilingi bilioni 15.


Waziri wa Fedha na Mipango Dokta Philip Mpango mara baada
ya kupokea gawio hilo la shilingi bilioni 15 kutoka benk ya
NMB ameishukuru benki hiyo na taasisi nyingine ambazo
zinakumbuka kutoa gawio kwa serikali.

Exit mobile version