Pipi zatumika kutibu Maji Wilayani Chemba Dodoma.

Licha ya kuwa Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi,lakini hali
duni inayosababishwa na uhaba wa Maji safi na Salama pamoja
na miundombinu katika baadhi ya maeneo Wilayani Chemba
unawatesa wakaazi wake.


Katika kutafuta ufumbuzi wa kunusuru Afya zao baadhi yao
wameamua kujivisha utabibu wa asili,kwani wakati wewe
ukinunua pipi kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo
kumumunya,katika wilaya ya Chemba ni tofaut kwani pipi hizo
hizo zinatumika kutibu maji,kama anavyoelezea mama huyu.


Katika upande wa miundombinu ya barabara hususani kwenye
madaraja bado ni chagamoto,kwani mvua kubwa zinaponyesha
kwa wingi hali huwa tete kutoka eneo moja kwenda jingine.

Exit mobile version