Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka viongozi
wa dini na wananchi kuomba huku wakichukua tahadhari
zinazotolewa na wataalamu wa afya ili kujikinga na maambukizi
ya virusi vya Corona.
RC Mwanri ametoa maelekezo hayo katika ibada maalum ya
kuombea mkoa na Taifa na kusema Corona haina imani
inakomba na imeleta taharuki kubwa watu wanahaha
wanapaniki dunia imekuwa kama senene wa kihaya.