TANZANIA haidaiwi 4.1 Bilioni na EIB Wizara ya mipamgo yakanusha.

Wizara ya Fedha na Mipango yakanusha taarifa inayosambaa mitandaoni ikidai kuwa Benki va Uwekezaji ya Ulaya EIB, naidai Tanzania dola za Kimarekani bilioni 4.1 (zaidi ya shilingi trilioni 10 za Kitanzania) na kwamba mwezi Januari, Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, aliomba mkopo mwingine kwenye Benki hiyo, lakini ilikataa kutoa mkopo huo kwa sababu haijalipwa deni kwa muda wa miezi 28.

Wizara hiyo imesema mtandao huo umekuwa ukitoa taarifa za uzushi, upotoshaji na uzandiki didi ya Wizara ya Fedha na Mipango na Serikali kwa ujumla huku lengo lake likiwa halifahamiki bayana.

“Tunawaomba watanzania na Jumuiya ya Kimataifa, mzipuuze taarifa hizo, ambazo hazina ukweli wowote na kwa vyovyote vile zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki isiyokuwa na sababu za msingi.”
#radio5fm

Exit mobile version