Wajasiriamali Wapewa Somo na Waziri Amina Salum Ali

Waziri wa Biashara na Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bi. Amina Salum Ali amewataka wajasiriamali nchini kutumia teknolojia ya kisasa kuzalisha bidhaa bora zenye viwango ambazo zitakidhi soko la ushindani.

Akizungumza kwenye kongamano la KCB JIAJIRI lililoshirikisha wajasiriamali zaidi ya elfu moja jijini DSM, Waziri Amina amesisitiza kwamba matumizi ya teknolojia katika kuzalisha bidhaa kuna mhakikishia mlaji usalama anapotumia bidhaa husika.

Aidha ametaka watanzania kujenga utamaduni wa kutumia bidhaa za ndani, akitolea mfano wa mataifa mengine yaliyozindua kampeni ya nchi zao kwanza, na kusema hata kwa hapa nchini inawezekana kuifanya Tanzania kwanza, kabla ya kununua bidhaa kutoka nchi nyingine.

Exit mobile version