Waziri awaita watakaosaidia nchi kupata mafuta bei rahisi.

Waziri wa Nishati Mhe Januari Makamba, ametoa wito kwa
Watanzania wote kutoa ushirikiano katika ununuzi wa mafuta
kwa kuwasiliana na wizara yake iwapo wana taarifa za namna
ya kupata mafuta ya bei rahisi.


Ametoa kauli bungeni hiyo leo Jumatano Aprili 13, 2022 katika
majadiliano ya bajeti ya waziri mkuu, ambapo amesisitiza
watakaopeleka taarifa hizo waihakikishie Serikali kuwa mafuta
hayo yatakuwa yanapatikana wakati wote.

Exit mobile version