Waziri Mkuu wa DRC ajiuzulu kupisha uteuzi mwingine.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Samy Badibanga ametangaza kujiuzulu.

Hatua hii imekuja baada ya rais Joseph Kabila siku ya Jumanne, kulihotubia bunge na kuahidi kumteua Waziri Mkuu mpya ndani ya saa 48.

Badibanga mwenye umri wa miaka 54 aliteuliwa katika nafasi hiyo mwezi Novemba mwaka 2016 baada ya jitihada za kuwepo kwa mazungumzo ya kisiasa chini ya mjumbe wa Umoja wa Afrika.

Baada ya kutiwa saini kwa mkataba wa kisiasa kati ya serikal na upinzani mwisho wa mwezi Desemba mwaka 2016 baada ya upatanishi, wa Maaskofu wa Kanisa Katoliki,ilikubaliwa kuwa Waziri Mkuu mpya ateuliwe kutoka upinzani.

Muda wa rais Kabila kukaa madarakani ulikamilika mwaka uliopita lakini kwa sababu ya mzozo wa kisiasa nchini humo, ameendelea kukaa madarakani baada ya Tume ya Uchaguzi kusema haina fedha za kuandaa Uchaguzi Mkuu.

Upinzani wamekuwa wakisema kuwa wanataka kupendekeza jina moja huku upande wa serikali ukisema kuwa upinzani kupendekeza majina matatu na rais kumteua mmoja.

Hata baada ya hotuba ya rais Kabila, wanasiasa wa upinzani wameonekana kutounga mkono na juhudi za rais Kabila kuwa Waziri Mkuu atapatikana baada ya  saa 48 na kupitisha uundwaji wa serikali ya mpito.

Exit mobile version