Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Kung’atuliwa

Mbunge mwenye ushawishi mkubwa nchini Ukraine amesema waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Oleksii Reznikov ataondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na mkuu wa ujasusi jeshini, kutokana na tuhuma za ufisadi jeshini.

Waziri huyo wa ulinzi wa Ukraine amekuwa akikabiliwa na shinikizo la kumtaka ajiuzulu, baada ya kuibuka tuhuma za ufisadi jeshini, lakini amekuwa akikaidi shinikizo hilo, akisema ataachia ngazi ikiwa tu atatakiwa kufanya hivyo na Rais Volodymyr Zelenskiy.

Hata hivyo, mbunge mmoja mwenye nguvu nchini Ukraine, David Arakhamia amesema jana jioni kuwa Reznikov angeondolewa kutokana na kashfa hiyo ya ufisadi ambayo imemlazimisha naibu wake kujiuzulu.

Arakhamia amesema vita vinaweka ushawishi katika sera zinazohusu wafanyakazi, na kwamba mkuu wa ujasusi jeshini Kyrilo Budanov angeteuliwa kuwa waziri mpya wa ulinzi. Mbunge huyo amesema waziri Reznikov atahamishiwa katika wizara nyingine, bila hata hivyo kubainisha muda yatakapofanyika mabadiliko hayo.

Exit mobile version