Programs


GOOD MORNING TANZANIA
 ni Kipindi cha Asubuhi kinachokuamsha na Uchambuzi wa Habari zote kubwa za Kisiasa, Kijamii, Uchumi, Teknolojia, Biashara na Michezo.

Kwenye Good Morning Tanzania utakutana na Mada Zinazojadiliwa Kila siku huku wewe ukiwa Mtoa Maoni lakini Pia Utakutanishwa na Mahojiano ya Moja kwa moja na Viongozi wa Kisiasa, Wachumi, Wataalamu wa Kiteknolojia, Viongozi wa Kijamii na Wanamichezo.

Kipindi hiki Kinaongozwa na SEMIO SONYO na ASHURA MOHAMED.

Ni kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi saa 4:00 Asubuhi.

MISHE MISHE ni Magazine Show ambayo unaweza kuiita Kapu la Kila Habari za Kila Mishe watu wa rika zote wanazozifanya kila Siku.

Ni Kipindi kinachobeba Habari za aina zote huku kikitoa elimu katika nyanja mbali mbali.

Vipengele vinavyopatikana katika Kipindi hicho ni kama Harakati za Usafiri, Nzito ya Leo, Kilingeni kwetu na Shushu ndimu mkata shombo.

Burudani ni sehemu ya Kipindi hiki hivyo kila siku unapata Ujazo wa Kila aina ya muziki kwenye Kipindi hiki.

Kipindi Kinaongozwa na MWANAISHA SULEIMAN na MWANGAZA JUMANNE huku Upande wa Burudani ukisimamiwa na DJNOEL255 

Usiache Kupata Uhondo huu kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 4:00 Asubuhi hadi Saa 7:00 Mchana.

FUNIKO BASE a.k.a SHOW LA KIBABE a.k.a SERIKALI YA MCHANA, Hiki ni Kipindi cha Burudani cha Tofauti na Vipindi vingine vya Burudani Tanzania.

Funiko Base ni Package ya Hot Entertainment Stories, Good Music, na Exclusive Interview.

Utakutana na Lock Nene ya Mastaa mbali mbali wakifunguka Stories ambazo hawazizungumzi pengine popote, Wakiwa ni Wasanii wa Nymbani Tanzania, Afrika na Dunia Nzima.

Vipengele Pendwa kwenye Funiko Base ni ISSUES ZA AFRIKA, MKONO WA DJ, 10 OF FAMES, NICHANE LIVE na STORY MOBB.

Kutana na Mtangazaji wake HAZUU na Good Music ikisimamiwa na DJKINGDAVID

Ni Kila Jumatatu hadi Ijumaa Saa Saba Kamili Mchana hadi Saa kumi Jioni. KARIBU KWENYE NOMA YA SERIKALI YA MCHANA


ANTENNA  ni kipindi cha jioni Kinachokutoa Kazini na Kukupeleka nyumbani huku Kikikuhabarisha na kukuondolea uchovu na mawazo yote ya kazini kukukaribisha nyumbani kwako ukiwa mpya.

Kipindi hiki kina mkusanyiko wa habari zote kubwa za siku na matukio gumzo kuanzia siasa, biashara, uchumi, michezo, mahojiano mbali mbali na burudani ya muziki mzuri.

Kipindi hiki kinaongozwa na watangazaji watutu ambao ni WILBERD KIWALE (Kiwa Strong), JOHANESS KINANILA  (Kid King) na FLORENSIA SHIRIMA (Flowie da Queen) Wote kwa Pamoja waite Mafundi wa kucheza na maneno.

Don’t Miss the show Wewe “KAA KWA KUTULIA TU” Jumatatu hadi Ijumaa Saa 10:00 jioni hadi Saa 12:30

RADIO5 NA MATUKIO, Hiki ni Kipindi Pendwa Tanzania chenye Mkusanyiko wa Matukio yote makubwa yaliyotokea kwa Kutwa nzima.

Kwenye Kipindi hiki utapelekwa Kihabari na Waandishi wetu waliosambaa kila Mkoa Tanzania huku Tukikuunganisha pia na undani wa Matukio makubwa yaliyojitokeza nchi za Nje.

Matukio ya Kijamii, Kiuchumi, Siasa na Utamaduni kwetu ni Habari Tu.

Ungana na TONNIE KAISOI kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia Saa 1:00 Usiku hadi Saa 2:00 Kamili Usiku akuunganishe na Matukio yote ya kutwa Nzima Uishi nayo.

RADIO FIVE NA MATUKI Ndipo Matukio yanapoishi, USIKOSE KUSIKILIZA

FIVE SPORTS Ni Kipindi Bora cha Michezo Nchini Tanzania Chenye Mkusanyiko wa Habari za Kimichezo zilizojitokeza kutwa nzima kote Duniani.

Katika Kipindi hiki Utasikia Mahojiano ya Moja kwa Moja na Wanamichezo kote Duniani huku ukiupata Uchambuzi Mnono kutoka kwa Wachambuzi Wanaoaminika Kwenye Michezo.

Kipindi hiki ndicho Kipindi Pekee cha Michezo Tanzania Kinachoongozwa na Mwanamke Mchezaji HILDA KINABO.


Ungana na FIVE SPORTS Kila Siku ya Jumatatu hadi Ijumaa Saa 2:00 Kamili Usiku hadi Saa 3:00 Kamili Usiku.

Mobile Sliding Menu