Siku moja baada ya korea kusema ilikua tayari kuzamisha meli yakubeba ndege za vita,Rais wa China ametaka kuwepo uvumilivu wakati mawasiliano ya simu na rais wa Marekani yakifanyika.

In Kimataifa

Rais wa China Xi Jinping ametaka kuwepo uvumilivu kutoka pande zote wakati wa mawasiliano ya simu na rais wa Marekani Donald Trump siku moja baada ya Korea kusema kuwa ilikuwa tayari kuzamisha meli ya kubeba ndege za vita ya Marekani.

Mawasiliano hayo ya simu ndiyo ya pili kati ya viongozi hao wawili tangu wakutane huko Florida mapema mwezi huu.

Ni ishara ya hofu ya China kuwa msukosuko kati ya Marekani na Korea Kaskazini utasababisha mzozo.

Siku ya Jumapili vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini vilisema kuwa jeshi la Korea Kaskazini lilikuwa tayari kuzamisha meli ya Marekani ya USS Carl Vinson, ambayo Marekani inasema itawasili katika rasi ya Korea siku chache zinazokuja.

Meli hiyo ilitumwa na Rais Trump huku onyo ikitolewa kuwa Marekani imepotza uvumilivu kwa mipango ya nuklia ya Korea Kaskazini.

ASANTE KWA KUSIKILIZA MIMI NI ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Safari ya Messi na Lamine Yamal Iliyotikisa Historia ya Soka

Soka lina uwezo wa kuandika simulizi ambazo hata waandishi wa riwaya hawawezi kuzibuni. Fainali ya Kombe la Dunia kati

Read More...

Serikali ya Marekani yaichangia Tanzania bilioni 2.63

Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Marekani milioni moja, sawa na takribani Sh. biliooni 2.63 ili kusaidia

Read More...

Tanzania, Marekani zasaini makubaliano ya Dola Bilioni 3.14 kuimarisha sekta ya afya

Serikali za Tanzania na Serikali ya Marekani zimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya ushirikiano katika sekta ya afya ya

Read More...

One commentOn Siku moja baada ya korea kusema ilikua tayari kuzamisha meli yakubeba ndege za vita,Rais wa China ametaka kuwepo uvumilivu wakati mawasiliano ya simu na rais wa Marekani yakifanyika.

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu