HARMONIZE NA TATOO MPYA MGONGONI.
Baada ya kumkosha Raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli sasa kwenye vichwa vya habari tena Tanzania ni Konde Boy #harmonize maarufu kama Jeshi.
kondeboy ameamua kuwaonyesha mashabiki zake mchoro mpya wa #tatoo yenye picha ya mnyama tembo kwenye mgongo wake.
Bado haijajulikana ni sababu zipi zimemfanya kuchora Tatoo hiyo lakini yawezekana ikawa ni katika maandalizi ya ujio wa album yake ya kwanza ambayo inatarajiwa kutoka mwezi huu.
Hata hivyo hivi karibuni umezuka mtindo wa wasanii kujiita majina ya wanyama Simba, Chui, Paka hii inawezekana kuwa utambulisho mwimgine wa mkali huyo wa Afro Pop anayesumbua kwa sasa Tanzania.




