Baada ya tetesi za muda mrefu kwenye mitandao ya kijamii kuhusu penzi la rappa wa kimarekani #lilwayne na mrembo mwenye asili ya India #LaTeciaThomas kuzagaa kwa muda mrefu, wawili hao wameamua kuweka wazi mapenzi yao.
Rappa Lil Wayne anaonekana amezama kwenye penzi zito na mrembo huyo baada ya kuonekana nae Wikiendi hii katika michezo ya kikapu (NBA All Stars Games) wakiwa wamegandana kama ruba.
Hata hivyo rappa huyo inawezekana ameziba masikio na kufa kimapenzi kwa binti huyu licha ya mashabiki zake kuonekana kutopendezwa na mrembo huyo.
Weezy aliungana na rappa #chancetherapper na #djkhaled wikiendi hii kushusha bonge la burudani wakati wa mapumziko katika mchezo wa NBA All Stars Games uliofanyika huko Chicago Nchini Marekani.



